Psalms 37:12-40


12 aWaovu hula njama dhidi ya wenye haki
na kuwasagia meno,
13 bbali Bwana huwacheka waovu,
kwa sababu anajua siku yao inakuja.

14 cWaovu huchomoa upanga
na kupinda upinde,
ili wawaangushe maskini na wahitaji,
kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu.
15 dLakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe,
na pinde zao zitavunjwa.

16 eBora kidogo walicho nacho wenye haki
kuliko wingi wa mali wa waovu wengi;
17 fkwa maana nguvu za waovu zitavunjwa,
lakini Bwana humtegemeza mwenye haki.

18 g Bwana anazifahamu siku za wanyofu,
na urithi wao utadumu milele.
19 hSiku za maafa hawatanyauka,
siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.

20 iLakini waovu wataangamia:
Adui za Bwana watakuwa
kama uzuri wa mashamba,
watatoweka,
watatoweka kama moshi.

21 jWaovu hukopa na hawalipi,
bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.
22 kWale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi,
bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.

23 lKama Bwana akipendezwa na njia ya mtu,
yeye huimarisha hatua zake,
24 majapojikwaa, hataanguka,
kwa maana Bwana
humtegemeza kwa mkono wake.

25 nNilikuwa kijana na sasa ni mzee,
lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa
au watoto wao wakiombaomba chakula.
26 oWakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti.
Watoto wao watabarikiwa.

27 pAcha ubaya na utende wema,
nawe utaishi katika nchi milele.
28 qKwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki
naye hatawaacha waaminifu wake.

Watalindwa milele,
lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.
29 rWenye haki watairithi nchi,
na kuishi humo milele.

30 sKinywa cha mwenye haki hutamka hekima,
nao ulimi wake huzungumza lililo haki.
31 tSheria ya Mungu wake imo moyoni mwake;
nyayo zake hazitelezi.

32 uWatu waovu huvizia wenye haki,
wakitafuta kuwaua;
33 vlakini Bwana hatawaacha mikononi mwao
wala hatawaacha wahukumiwe
kuwa wakosa wanaposhtakiwa.

34 wMngojee Bwana,
na uishike njia yake.
Naye atakutukuza uirithi nchi,
waovu watakapokatiliwa mbali,
utaliona hilo.

35 xNimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi
kama mwerezi wa Lebanoni,
36 ylakini alitoweka mara na hakuonekana,
ingawa nilimtafuta, hakupatikana.

37 zWatafakari watu wasio na hatia,
wachunguze watu wakamilifu,
kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.
38 aaLakini watenda dhambi wote wataangamizwa,
mafanikio yao yatakatiliwa mbali.

39 abWokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana,
yeye ni ngome yao wakati wa shida.
40 ac Bwana huwasaidia na kuwaokoa,
huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi,
kwa maana wanamkimbilia.
Copyright information for SwhNEN